Stay updated with breaking news from Shabari jayanti. Get real-time updates on events, politics, business, and more. Visit us for reliable news and exclusive interviews.
Tajiri mkubwa sana barani Afrika Aliko Dangote yuko kwenye mazungumzo na makampuni makubwa ya mafuta ulimwenguni, ikiwajuhudi ya kufadhili kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Nigeria. ....
Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden Jumatano umeanza kuwajulisha magavana wa majimbo pamoja na waratibu wa wakimbizi kote nchini kuhusu idadi ya wakimbizi wanaotarajiwa kwa kila jimbo miongoni mwa karibu 37,000 kutoka Afghanistan. ....
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres, Jumapili amelaani kile kinachotajwa kama mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea, na kuwasihi wanajeshi waliosema wamefanya mapinduzi hayo na kuchukua madaraka, kumuachilia huru rais Alpha Conde. ....
Serikali ya Tanzania Jumapili imesimamisha uchapishaji wa gazeti moja la kibinafsi kwa siku 30, baada ya kumhusisha mtu mwenye silaha, aliyetajwa na maafisa wa usalama kama“gaidi” ambaye aliua watu wanne, na chama tawala cha nchi hiyo. ....
Serikali iko katika shinikizo la kufungua tena shule, kwanza, kwa sababu za kielimu, lakini pia ikizingatia madhara ya kiuchumi ya kufunga shule za wamiliki binafsi ambao wanakabiliwa na hatari ya mali zao kuuzwa ili waweze kulipa mikopo ya benki, limeandika gazeti la The East African, Jumapili. ....