comparemela.com

Latest Breaking News On - Soccer europe friday - Page 2 : comparemela.com

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 23 07 2021: Kane, Mbappe, Pogba, Varane, Kessie, Hazard, Xhaka

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 23.07.2021: Jadon Sancho ,Kane, Mbappe, Pogba, Varane, Kessie, Hazard, Xhaka 23 Julai 2021, 06:45 EAT Chanzo cha picha, Getty Images Winga wa Uingereza Jadon Sancho anasema kujiunga na Manchester United ni ndoto inayotimia baada ya kumaliza uhamisho wake wa pauni milioni 73 kutoka Borussia Dortmund. Sancho ndiye mchezaji wa pili mwenye gharama ya juu zaidi wa England wakati wakati wote nyuma ya mwenzake mpya wa United Harry Maguire. Anajiunga na United kwa mkataba wa miaka mitano. Nitashukuru Dortmund kila mara kwa kunipa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, ingawa siku zote nilijua kwamba nitarudi England, Sancho, 21, alisema Nafasi ya kujiunga na Manchester United ni ndoto iliyotimia na siwezi kungojea kunawiri kwenye Ligi ya Premia.

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 16 07 2021: Pellegrini, Abraham, Salah, Varane, Lingard, Vlahovic, Ajer, Emerson

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 16.07.2021: Pellegrini, Abraham, Salah, Varane, Lingard, Vlahovic, Ajer, Emerson 16 Julai 2021, 06:45 EAT Imeboreshwa Saa 2 zilizopita Chanzo cha picha, Reuters Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anawataka viongozi wa klabu kumsajili mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah,29, anayekipiga Liverpool ikiwa mchakato wa kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe utakwama msimu huu wa joto. (Fichajes - in Spanish) Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 23 ambaye the blues pia wameashiria kuwa tayari kumuuza kwa Tottenham na Inter milan.Chelsea wanawalenga mshambuliaji wa Spurs na England Harry Kane mwenye umri wa miaka 27 na Romelu Lukaku wa Inter na Ubelgiji (Telegraph

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 09 07 2021: Traore, Bellerin, Pogba, Olsen, Lenglet

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 09.07.2021: Leonardo Bonucci,Traore, England,Italy, Pogba, Olsen, Lenglet,Euro 2020,Wembley 9 Julai 2021, 06:53 EAT Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Paul Pogba Leonardo Bonucci anasema Italia haiogopi kushiriki fainali ya Euro 2020 kwenye ardhi ya Uingereza wakati pande hizo mbili zitapambana Jumapili. Italia iliifunga Uhispania kwa mikwaju ya penati baada ya nusu fainali ya kuvutia kwenye Uwanja wa Wembley uliokuwa na vurugu Jumanne. Ingawa kutakuwa na umati wa Waingereza, itatupa motisha zaidi, Bonucci alisema. Mashabiki wapatao 1,000 wa Italia wataruhusiwa ndani ya Wembley kutazama mchezo huo. Paris St-Germain wanaamimi kwamba watamnasa Paul Pogba kwa bei chee ya £50m wakati huu wakiendelea kutupa ndoano zao kujaribu kumnasa kiungo huyo wa Manchester United na Ufaransa. (Star)

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 08 07 2021: Haaland, Guardiola, Richarlison, Jorginho, Ramos, Goretzka

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.07.2021: Ramos, Haaland, Guardiola, Richarlison, Jorginho, Ramos, Goretzka 8 Julai 2021, 06:46 EAT Imeboreshwa Saa 6 zilizopita Chanzo cha picha, PSG/twitter Paris St-Germain imemsajili Sergio Ramos kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya mchezaji huyo kuondoka katika klabu yake ya miaka mingi Real Madrid. Ramos , 35 aliondoka Madrid baada ya miaka 16 wakati kandarasi yake ilipokamilika mwisho wa mwezi Juni. Mchezaji huyo ambaye ameichezea mara nyingi zaidi timu yake ya taifa kushinda mchezaji yeyote yule ,ameshinda mataji matano ya La liga na mataji manne ya kombe la klabu bingwa akiichezea Real Madrid. Mwenyekiti wa PSG Nasser al khelafi alisema: Paris inamkaribisha mchezaji maarufu wa enzi yetu .

© 2025 Vimarsana

vimarsana © 2020. All Rights Reserved.