Tanzania-Uganda: Ramani ya Afrika mashariki ingekuwa tofauti na ilivyo sasa iwapo Amin angeshinda vita vya Kagera
Saa 8 zilizopita
Chanzo cha picha, TANZANIAGOV
Vita vya Uganda-Tanzania, vinavyojulikana nchini Tanzania kama Vita vya Kagera na nchini Uganda kama vita vya Ukombozi vilihusisha Uganda na Tanzania kati ya Oktoba 1978 hadi Juni 1979. Matokeo yake yalikuwa kutimuliwa kwa Idi Amin madarakani na mwezi huu wa Juni ambapo vita viliisha tunakupakulia kumbukumbu za chanzo na matokeo ya vita hivyo .Leo tunaanza na jinsi mzozo huo ulivyoanza . Matokeo yake endapo yangeipa Uganda ushindi ,yangebadilisha kabisa ramani ya afrika mashariki kama ilivyo sasa .
Chanzo kikuu cha mapigano hayo kilitokana na hatua ya rais wa Uganda wa wakati huo Idi Amin kutangaza kwamba eneo la Kagera lilifaa kuwa sehemu ya Uganda.Hatua hiyo ilimlazimu rais wa Tanzanzia wakati huo hayati Julius Nyerere kutangaza vita dhidi ya Uganda na baadaye kusaidia kumuondoa Amin madarakani .