Iraq:Baada ya kuondoka Afghanistan,Marekani sasa yapanga kuondoa majeshi yake Iraq
27 Julai 2021, 05:59 EAT
Chanzo cha picha, ANADOLU AGENCY
Rais wa Marekani Joe Biden anasema vikosi vya Marekani vitamaliza misheni yao ya mapigano nchini Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, lakini wataendelea kutoa mafunzo na kuwashauri wanajeshi wa Iraq.
Tangazo hilo lilikuja baada ya Bwana Biden kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhimi katika Ikulu ya White House.
Hivi sasa kuna wanajeshi 2,500 wa Marekani nchini Iraq wakisaidia vikosi vya nchi hiyo kukabiliana na wapiganaji waliobaki wa kundi la Islamic State.
Idadi ya wanajeshi wa Marekani inaweza kusalia jinsi ilivyo lakini hatua hiyo inaonekana kama jaribio la kumsaidia Waziri Mkuu wa Iraq.