Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 13.07.2021: Varane, Bellerin, Kane, Haaland, Jesus
13 Julai 2021, 06:36 EAT
Imeboreshwa Saa 2 zilizopita
Chanzo cha picha, Getty Images
Vigogo wa jiji la London na klabu bingwa ya Ulaya Chelsea inatarajia kutangaza ofa kubwa ili kumnasa mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Erling Braut Haaland. (Daily Star)
Hector Bellerin ameiambia Arsenal kuwa anataka kuondoka wakati wa dirisha la usajili majira ya joto. Mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi mwenye miaka 26, ambaye ni mchezaji wa muda mrefu wa kikosi cha kwanza cha Mikel Arteta ana matumaini ya kuhamia Inter Milan. (Metro)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Antoine Griezmann, 30, lakini wana nia na mshambuliaji wa Norway na Borussia Dotmund Erling Braut Haaland, 20, na nahodha wa Tottenham England Harry Kane. (The Sun)