Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 16.07.2021: Pellegrini, Abraham, Salah, Varane, Lingard, Vlahovic, Ajer, Emerson 16 Julai 2021, 06:45 EAT Imeboreshwa Saa 2 zilizopita Chanzo cha picha, Reuters Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anawataka viongozi wa klabu kumsajili mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah,29, anayekipiga Liverpool ikiwa mchakato wa kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe utakwama msimu huu wa joto. (Fichajes - in Spanish) Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 23 ambaye the blues pia wameashiria kuwa tayari kumuuza kwa Tottenham na Inter milan.Chelsea wanawalenga mshambuliaji wa Spurs na England Harry Kane mwenye umri wa miaka 27 na Romelu Lukaku wa Inter na Ubelgiji (Telegraph