Ghasia za Afrika Kusini:Ndani ya wiki ya machafuko na uporaji jijini Durban 29 Julai 2021 Chanzo cha picha, AFP Wiki mbili baada ya Afrika Kusini kukumbwa na wimbi la ghasia na uporaji - matukio mabaya zaidi ya vurugu tangu ujio wa demokrasia mnamo 1994 - vizuizi vya muda mfupi na majaa ya takataka katika jiji la bandari la Durban vimeondolewa. Lakini wanajeshi wanaendelea kufanya doria katika vitongoji vilivyoharibiwa na wiki ya machafuko ambayo iliwaacha watu zaidi ya 300 wakiwa wamekufa. "Kila kitu kimeenda. Sina bima. Nina wasiwasi juu ya siku zijazo za Afrika Kusini. Nina wasiwasi juu ya maisha ya baadaye ya watoto wangu," alisema mjasiriamali Dawn Shabalala, ambaye maduka yake manne madogo yaliporwa - hadi bomba la maji na nyaya za umeme