Dola Milioni 100 kuwasaidia wakimbizi wa Afghanistan Rais wa marekani Joe Biden ameidhinisha dola milioni 100 katika kushughulikia dharura ya wakimbizi inayohusiana na hali nchini Afghanistan Katika taarifa yake, Ikulu ya White House imesema fedha hizo zitatoka kwenye mfuko wa dharura na ule wa kusaidia wakimbizi kwa lengo la kukabiliana na dharura ambayo haikutarajiwa ya wakimbizi, wahanga wa mzozo na baadhi ya watu ambao wako hatarini kutokana na hali ilivyo nchini Afghanistan. Fedha hizo zitawasaidia wale wanaoomba visa maalumu SIVs, ambapo karibu raia 20,000 wa Afghanistan walikuwa wakifanya kazi ya ukalimani na kazi nyingine kuisadia Marekani wakati wa vita na sasa wanahofia kuadhibiwa na Taliban. Fedha hizo zinaweza kukusanywa kupitia michango ya ufadhili wa mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na yale ya Marekani, iliongeza taarifa hiyo.