Serikali iko katika shinikizo la kufungua tena shule, kwanza, kwa sababu za kielimu, lakini pia ikizingatia madhara ya kiuchumi ya kufunga shule za wamiliki binafsi ambao wanakabiliwa na hatari ya mali zao kuuzwa ili waweze kulipa mikopo ya benki, limeandika gazeti la The East African, Jumapili.