comparemela.com

Latest Breaking News On - Spoken july - Page 1 : comparemela.com

Polisi wavunja mkutano wa Chadema, 30 wakamatwa

HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limevunja mkutano wa kujadili Katiba Mpya ulioandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) pamoja na kuwakamata makada 30 kwa madai ya kufanya mkutano wa hadhara bila kibali. Hata hivyo, Chadema wamepinga madai hayo ya kufanya mkutano wa hadhara, wakisema ulikuwa in mkutano wa ndani ambao kwa utaratibu hauhitaji kibali cha Polisi. Akizungumza kwa simu leo Jumamosi Julai 17,2021, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng anzi alisema wamevunja mkutano huo kwa kuwa haukuwa na kibali. Ni kweli tumezuia mkutano ulioandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema kwa ajili ya kudai Katiba mpya kwa kuwa hawakutoa taarifa Polisi na sisi kuwaruhusu kufanya mkutano huo, alisema Kamanda Ng anzi.

© 2025 Vimarsana

vimarsana © 2020. All Rights Reserved.