Juneteenth National Independence Day itakuwa inaadhimishwa Juni 19 ya kila mwaka. Ni siku katika mwaka 1865 wakati wanajeshi wa muungano walipoliarifu kundi la watumwa weusi kwenye jimbo la Texas juu ya uhuru wao miaka miwili na nusu baada ya Rais Abraham Lincoln kutia saini tangazo la ukombozi
Naftali Bennett ameapishwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Israel
14 Juni, 2021
Shirikisha
share
Print
Bennett atakuwa Waziri Mkuu kwa miaka miwili kwa mujibu wa makubaliano yasiyo ya kawaida ya kushirikiana madaraka miongoni mwa vyama vinane vya kisiasa vyenye mtizamo mdogo wa pamoja isipokuwa kutaka kumaliza uongozi wenye mzozo wa Netanyahu
Serikali mpya ya Israel iliapishwa Jumapili na kumaliza utawala wa miaka 12 wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kumfanya Naftali Bennett, mkuu wa chama kidogo cha kidini kuwa kiongozi mpya wa taifa la wayahudi.
Bennett atakuwa Waziri Mkuu kwa miaka miwili kwa mujibu wa makubaliano yasiyo ya kawaida ya kushirikiana madaraka miongoni mwa vyama vinane vya kisiasa vyenye mtizamo mdogo wa pamoja isipokuwa kutaka kumaliza uongozi wenye mzozo wa Netanyahu.
Algeria inafanya uchaguzi wa bunge Jumamosi wakati vuguvugu la maandamano likisihi wapiga kura kususia huku kukiwa na wasi wasi kwamba taifa hilo la Afrika kaskazini linaweza kujikwamua kutoka kwenye janga la kisiasa na kiuchumi.
Pande hizo mbili zinatambua uzito wa hali hiyo na zinasisitiza dharura ya kufafanua mazingira ambayo shambulizi hili lilifanyika, mawaziri wa mambo ya nje wa Chad na CAR walisema katika taarifa ya pamoja Jumanne jioni
Bachelet alisema hayo wakati wa kikao maalum cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kilichoombwa na Organisation of Islamic Conference, kundi la mataifa ya kiislam kutaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike kuhusu masuala ya haki za binadamu huko Israel, Gaza na ukingo wa magharibi