Wake wa marais: Mfahamu mke wa rais wa DRC Denise Nyakeru Nkana Tshisekedi
Dinah Gahamanyi
Chanzo cha picha, Denise Nyakeru/Facebook
Maelezo ya picha,
Hadithi ya maisha ya Bi Denise Tshisekedi imekuwa na kusikitisha kwa upande mmoja na upande mwingine ya kutia moyo
Ni watu wenye ushawishi katika uongozi wa kila siku wa nchi zao, hata hivyo si kila siku utasikia juu ya maisha yao na vipawa vyao. Hawa ni wenza wa marais, ambao baadhi yao ni wanasiasa na wanaharakati ambao wamekuwa bega kwa bega katika safari za kisiasa za wenza wao mpaka kushika hatamu za madaraka. Wiki hii tunakuletea mfululizo wa makala kuhusu wenza wa marais katika eneo la Afrika Mashariki na Maziwa Makuu ambapo leo