Mgogoro wa Ethiopia:Kwanini mamia ya malori yamekwama? bbc.com - get the latest breaking news, showbiz & celebrity photos, sport news & rumours, viral videos and top stories from bbc.com Daily Mail and Mail on Sunday newspapers.
Waridi wa BBC- Ninajilaumu kwa kupewa talaka
Anne Ngugi
Chanzo cha picha, Gladys
Bi Gladys Kagendo , mama ya mtoto mmoja , mnamo Juni mwaka huu alitimu miaka 30 .Ila katika umri huu ambao bila shaka bado yuko kwenye ujana wake , tayari alikuwa amefunga ndoa , kupata ujauzito na kupewa talaka yote haya yakifanyika katika kipindi cha miezi 7 pekee .
Hatahivyo licha ya hali inayomkabili ameamua kujilaumu yeye mwenyewe kwa kuwa alichangia pakubwa sababu zilizoangamiza ndoa yake . Nadhani kuwa matukio katika maisha yangu ya ndoa , yamekuwa ni somo kuu kwangu . Sitaki kulaumu mtu yeyote kwa sababu naamini kila mhusika alikuwa na kosa moja au jingine ,kwa kila aliye kwenye ndoa ni muhimu kufahamu ni kipi anachoweza kuvumilia na ni kipi hawezi , tuwache kurushiana lawama za ni huyu alifanya kosa hili na kadhalika anasema Gladys