Mazungumzo ya Afghanistan yakamalika Doha bila ufumbuzi
Mazungumzo ya karibuni kati ya serikali ya Afghanistan na Taliban mjini Doha yamemalizika bila mafanikio hata baada ya kiongozi mkuu wa wanamgambo hao wa itikadi kali kusema anaunga mkono kwa dhati suluhisho la kisiasa
Wawakilishi waandamizi wa serikali ya Kabul akiwemo kiongozi wa Baraza Kuu la Maridhiano ya Kitaifa Abdullah Abdullah walikuwa Doha kwa siku mbili za mazungumzo mazito wakati Taliban ikiendelea na operesheni yake kali ya kuyakamata maeneo nchini Afghanistan. Abdullah Abdullah alikuwa na kauli fupi tu baada ya mazungumzo ya jana Ningetarajia kazi kumalizika usiku huu na ilifanyika, lakini tulikuwa na majadiliano mazuri. sawa? ahsante . Alisema Abdullah Abdullah