Madkatari wakamatwa Myanmar
Shirikisha
Print
Jeshi la Myanmar limewakamata na kuwazuia madaktari kadhaa kutokana na kuunga mkono maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi ulilochukua madaraka.
Wengi waliozuiliwa wanasemekana kuwa na kliniki binafsi ambako wanasaidia kwenye juhudi za kutibu wagonjwa wa corona, wakati taifa hilo likikabiliana na wimbi jipya la maambukizi.
Tangu jeshi lilipofanya mapinduzi dhidi ya utawala wa kiongozi wa kiraiya Aung San Suu Kyi mwezi Februari. Ghasia na maandamano yaliyofuata yameathiri vita dhidi ya corona, wakati wanaharakati wakisema kuwa madaktari waliokamatwa ni kutokana na kupinga mapinduzi hayo.
Alhamisi Myanmar imetangaza visa vipya 6,000 vya corona baada ya kuripoti vifo 286 hapo awali. Wauguzi pamoja na wafanyakazi wa vyumba vya kuhifadhia maiti wanasema kuwa idadi hiyo huenda ikawa kubwa zaidi kwa kuwa maeneo ya kuchoma miili yameelemewa.