Latest Breaking News On - Darfur west - Page 1 : comparemela.com
Wanawake wapitia mateso Darfur
Shirikisha
Print
Wanaharakati wa haki za wanawake kutoka magharibi mwa Sudan wanasema kuwa mamia ya wanawake waliokoseshwa makazi kutokana na mapigano huko Darfur wanapitia hali ngumu ya maisha. Hali hiyo ni kufuatia mapigano ya kikabila kwenye mji wa Al Geneina Darfur magharibi, wakati wakisemekana kupitia hali ya wasi wasi pamoja na msongo wa mawazo kutokana na jukumu kubwa la kulea watoto bila kuwa na waume zao.
Mapigano hayo yaliozuka Aprili yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 200 huku idadi sawa na hiyo iwakiwa wamejeruhiwa. Maelfu ya familia zimepewa hifadhi kwenye mashule, misikiti pamoja na majengo ya serikali.
Darfur-west
Fighting-it-april